VURUGU kubwa zilitokea jana jijini Dar es Salaam, katika mkutano Mkuu wa Halmashauri kuu ya Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), wakati wa kujadili rufani iliyowasilishwa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Hamad Tao kupinga kusimamishwa kwake.
Kutokuelewana huko kati ya mwenyekiti wa TLP, Dk. Augustino Mrema,wanachama na Tao wakati akiwasilisha rufani hiyo ambapo licha ya kupewa mda kujitetea ndipo alipoanza kujadili kiti ambacho hakukieleza katika rufani hiyo.
“Tao unatakiwa kueleza kile ambacho umekiwasilisha kwa njia ya maandishi na sio kama unavyo fanya kuongea ambayo hukuyawasilisha,”alisema Victor Limo Katibu Mipango wa TLP.
Hata hivyo Tao aliendelea kueleza kuhusu mapato na matumizi ya ndani ya TLP ambapo alidai ndio sababu ya yeye kuenguliwa na mkutano mkuu wa chama kwa kudai kujua.
“Chama chetu kinaendeshwa kidikiteta na mwenyekiti watu,hata ukitaka kujua mapato na matumizi huwezi pata nah ii nduio sababu ya nyinyi (wajumbe) kunitoa mimi katika uongozi lakini nawahakikishia kuwa mtawafukuza wengi kwa hili,” alisema Tao.
Baada ya kauli hiyo ndipo mabaunsa wa TLP waliokuwapo katika ukumbi huo kumtoa kwa nguvu huku ukumbi wote ukizizima makelele kuashiria kikomo cha uongozi wa Tao.
Kwa upande wake Dk. Mrema alisema kuwa Tao amekuwa akikiyumbisha chama kwa kipindi kirefu na sasa umefika wakati wa kuwaachia wengine kukiongoza ambao watakuwa na uchungu na maendeleo ya TLP.
“Nawaomba wanachama kutupilia mbali rufani ya Tao kwni amekiingiza chama katika migogoro na kukirudisha nyuma kwa kipindi kirefu sasa na umefika wakati way eye kuwa mwanachama tu na sio tena kiongozi kwani anaonekana kuwa anatumiwa na watu kutuweka hapa tulipo sasa,”alisema Dk. Mrema
Dk. Mrema aliongeza “Kwa kuwa mimi ndiye niliyemteua Tao kuwa naibu katibu mkuu hivyo basi namamlaka ya kumuondoa nyadhifa hiyo na kama atataka asubiri uchaguzi mkuu mwaka 2014 naye agombee kwa juhudi zake na kama atashinda ndio atuongoze lakini kwa sasa utupishe”.
0 comments:
Post a Comment