MWANAFALSAFA ambaye anafahamika zaidi kama Mwana FA, sasa ameamua kuandika mashairi yaliyotokana na wimbo wa taarab ambao uliimbwa na wasanii wakongwe wa muziki huo kutoka Tanzania Bara na Visiwani.
Staa huyo ambaye sasa anatamba na video ya Unanijua Unanisikia ameamua kumshirikisha msanii Linah kutoka THT ambaye naye kwa upande wake amesimama vilivyo katika nafasi hiyo.
Mwana FA alisema kuwa wimbo huo unafanana kabisa na zile nyimbo walizoimba wasanii wakongwe wa taarabu hapa nchini aliowataja kwa majina ya Siti Binti Saad, Malika pamoja na Bibi Kidude.
Wimbo huu kwenye chorus ameimba Linah na kurudia kwa melodi ile ile na kisha Mwana FA akaunganisha katika mashairi ya nyimbo hizo. Gitaa limepigwa na mmoja wa walimu wa muziki THT Cadinal Gento na biti ameisimamia Marco Chali kutoka MJ Records.
0 comments:
Post a Comment