MWANADADA anayetesa katika Komedi Bongo, Mai Ali Mai Dread, amelazimika kuikimbia kambi ya kundi lake la Vituko Show iliyopo jijini Mbeya akidai imejaa majungu.
Msanii kwa sasa anafanya kazi na Bongo Super Stars Comedy.
Nimekimbia kambi kwa sababu ya majungu, si unajua wanawake tukiwa pamoja? Lazima majungu yawepo. Ni balaa fulani hivi limeingia, alisema Mai Dread.
Awali nilipokuwa na akina Asha Boko, Bi. Rehema na wengineo, tulifanya kazi vizuri tu, lakini walivyoingia wasichana tu, mambo ya wivu yakaanza.
Msanii huyo amedai kuwa kutokana na yeye kuwa na mahusiano mazuri na uongozi, basi chuki zilianza kiasi cha kusababisha ugomvi wa mara kwa mara.
Anasema alitakiwa aendelee kuwepo kwenye kikundi hicho hadi Februari mwakani, lakini ameona bora atoke mapema.
Jitihada za kuzungumza na viongozi wa kundi lake zimegonga mwamba kwani hakuna kiongozi aliyekuwa tayari kufafanua suala hilo.

0 comments:
Post a Comment