Mkurugenzi wa Mamlaka ya hali ya hewa Agnes Kigazi
Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania imethibitisha kwamba leo huko Sumatra Indonesia kumetokea tetemeko maarufu kama Tsunami chini ya bahari ambapo hii hali inatarajiwa kutengeneza mawimbi ya Tsunami ambayo yanatarajiwa kufika kwenye pwani ya Tanzania hasahasa sehemu za Mtwara kuanzia saa 11 jioni leo.
Mvua zinazoendelea kunyesha Dar.
Mamlaka hiyo imesema “tunaomba wananchi kuchukua tahadhari na kufatilia taarifa kwenye vyombo vya habari kufahamu hali inaendeleaje kwa sababu tutakua tunatoa taarifa kila wakati, tunategemea mawimbi hayo kuwa ni mita moja nukta mbili, kama uko sehemu ambayo iko tambarare mawimbi yanaweza kuingia ndani zaidi lakini kama kuna muinuko, inaweza isiathiri.
0 comments:
Post a Comment