BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Saturday, July 10, 2010

Hemedi Ajipanga Upya

HEMED (PHD)

thazealottz  ilibahatika kukutana na msanii aliyeng'aa sana kwenye shindano la tusker project fame, wengi wanamjua kwa jina la Hemedi aka Handsome Boy. Hemedi baada ya kumaliza mashindano ya tusker project fame alianza kujishughulisha na muziki bongo wa kizazi kipya. Msanii huyo aliachia single iliyomtambulisha iitwayo 'Ninachotaka' iliyofanya vizuri kwenye chati.
Hemedi aliweka wazi sababu yake kubwa ya kupotea kwenye game kwa muda mrefu,kuwa ni kwenda shule kumaliza elimu yake.Mfano mkubwa sana wa kuigwa na wasanii wenzake na Jamii kwa ujumla kwani anatambua umuhimu wa elimu.
Hemedi juzi kati alijiingiza kwenye mashindano ya kucheza 'serebuka' ambapo kwa kupitia twisti kali aliloonyesha,alifanikiwa kufanya vizuri sana na hata kukonga nyoyo za mashabiki japokuwa hakulitwaa taji hilo.
Hemedi ana machache tu ya kusema kufuatia ujio wake mpya, 'Kwa mafans wangu,ni kwa sababu yenu napika vitu studio na nina ahidi kitatoka kitu cha ukweli sana! Mkae tayari kujipangusaa, Raaah Raaah!'

0 comments: