BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Monday, July 19, 2010

LINNAH MSANII WA BONGO FLAVA ANAYETAMBA NA KIBAO CHAKE ATATAMANI MPATE KWA UNDANI SASA..

Alizaliwa kwa jina la Estelinah Petter Sanga ....lakini kimuziki mwenyewe anapenda ajulikane kama 'Linah' mwenye umri wa miaka 19 ni mgeni katika tasnia ya muziki akiwa anatingisha na kibao chake 'Atatamani' huku akifanya vema katika wimbo alioshirikishwa na Barnabas 'Wrong number'.

Lakini kutokana na kibao matata ambacho alikiimba kimeweza kukonga nyoyo za mashabiki wengi. "Atatamani ni wimbo ambao unapendwa sana na wanadada, lakini pia wimbo huu unapendwa sana na wanaume pia kwakuwa ni kitu ambacho kinaigusa jamii yote kwa ujumla" anasema.

Mwenyewe anasema wimbo huo, halikuwa wazo lake..bali mashairi ya wimbo huo yalitoka kwa msanii mwenzake Amini ambaye naye pia ni uzao kutoka nyumba ya vipaji Tanzania 'THT'.

"Amini alikuwa akiuimba wimbo huu muda mwingi na tulipokuwa katika mazoezi nilipouimba alinikubali kwa kuwa nilikuwa naumudu vyema, hivyo akamweleza boss kwamba ni vema kama nikiimba mimi kwani ninafaa zaidi, ndipo nilipoingia studio na kuurekodi. 

LINAH AKIWA NA AMINI

"Katika wimbo huu maudhui yaliyomo ndani yake ni kama yanafanana na kisa ambacho kilishawahi kunitokea mimi mwenyewe, lakini nilishangaa baada ya Amini kunipa yale mashairi nilihisi ameniona undani wangu.

Mrembo huyu aliyeanzia muziki kanisani tangu alipokuwa mdogo akiwa ni mtoto wa Mchungaji Petter Sanga wa kanisa la Glory of Christ anasema kuwa wazazi wake hawana tatizo na juu ya ulokole wao, wamekubaliana na mtoto wao ya kwamba atimize ndoto zake za kuwa mwanamuziki mkubwa wa kike.

"Wazazi wangu hawana tatizo na uimbaji wangu,kiukweli naweza kusema wamenipa baraka zao zote " anasema.

Binti huyu ambaye alisoma Msigani Sekondari ya Mbezi Louis iliyopo jijini Dar es Salaam anasema kwamba hivi sasa kuna wimbi kubwa sana la wasichana ambao wamejiingiza katika uasherati na utegemezi hali inayozidi kuwakandamiza katika dimbwi na umasikini na maradhi.

"Tusiwe tegemezi, wengi wetu wamekuwa wakijirahisisha kwa wanaume ili waweze kuwa na maisha mazuri, lakini mwisho wa yote ni kuzidi kujikandamiza katika maisha ya dhiki mbeleni" Anachokieleza mdada huyu ni kwamba wasichana wengi ni wavivu na wanapenda kujibweteka.

0 comments: