BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Monday, July 19, 2010

Mainda, Johari Wapikwa Pamoja

Vincent Kigosi almaarufu kama Ray ameondoa kile kinachosemekana kitaa kuwa yuko ndani ya bifu kubwa na waigizaji Ruth Suka maarufu kama Mainda na Blandina Chagula, Johari, baada ya kuwashirikisha kwenye filamu mpya iitwayo Bed Rest. Miezi iliyopita iliripotiwa kuwa muigizaji huyo ameingia kwenye bifu na waingizaji hao kwasababu zilizoelezwa kuwa ni za kimapenzi.



Akiongea na vyombo vya habari, Ray alieleza hakuna kitu kama hicho na anamshukuru Mungu kwa kumpa moyo wa uvumilivu na kutojali yanayosemwa.
‘Mimi ninaangalia kazi, na namshukuru Mungu ninaendelea kufanya vizuri. Hakuna tatizo kati yangu na Johari wala Mainda na ndio maana tunatoa filamu nyingine ya Bed Rest, iliyoandaliwa na RJ Company ambayo johari na mimi ni wakurungenzi’,alisema Ray.
Ray alisema safari hii ametoka na story itakayoacha simulizi kwa atakaye angalia.
‘Ina hadithi nzuri na tumewashirikisha nyota mahiri na chipukizi ambao wana uwezo mkubwa’ ,alisema Ray. Aliwataja washiriki wengine walioigiza kwenye filamu hiyo kuwa; Ndumbagwe,They naNurdin  Mohamed chekibundi.

0 comments: