BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Wednesday, December 15, 2010

MARLAW,CHEGE KUTUMBUIZA BSS IJUMAA.



NYOTA kadhaa wa muziki wa kizazi kipya wakiwemo Marlaw, Diamond, Chege na Mh Temba watatumbuiza katika fainali ya kumsaka kinara wa shindano la ‘Kilimanjaro Bongo Star Search 2010’ kwenye ukumbi wa Mlimani city jijini Dar Es Salaam ijumaa.

 Ritha Paulsen na Meneja wa TBL.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam jana, mkurugrnzi  wa kampuni ya Benchmark Production inayoandaa shindano hilo, Ritha Paulsen, aliwataja nyota wengine watakao tumbuiza siku hiyo kuwa ni Mwasiti, Joh makini, Imani na Cindy kutoka nchini Uganda.
Alisema kuwa fainali hizo zitaoneshwa na moja kwa moja na kituo cha televisheni cha ITV kuanzia saa 1:00 usiku na maandalizi yote yamekamilika.
Nyota watano walioingia fainali na kuwania zawadi ya Kwanza ya  kitita cha Sh. Milioni 30 ni Bella Kombo mwenye namba BSS 02, joseph Payne BSS 07, Mariam Mohamed BSS 17, James Martin BSS 14 na Waziri Salum ambaye ni mshiriki namba BSS 11.
 Washiriki wakionesha zawadi ya mshindi wa kwanza.

Mshindi wa pili atapata Sh. Milioni 10 huku watatu akitarajiwa kuzoa Sh. Milioni tano.
Ritha alisema zawadi ya kwanza imetolewa na wadhamini wakuu wa shindano hilo, kampuni ya bia ya TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro, wakati zawadi ya mshindi wa pili imetolewa na kampuni ya huduma ya simu za mkononi ya Airtel.
 Tano bora ya BSS 2010.

Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George kavishe, alisema kuwa kampuni yake imeungana na Benchmark katika shindano hilo kwa nia ya kuibua vipaji vya muziki wa Tanzania.
Bella Kombo na joseph Payne  

0 comments: