BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Saturday, September 17, 2011

Baada ya Ukimya wa Miaka 2..Mwana FA kuja na album...


MWANAFALSAFA wa mashairi ya muziki nchini Hamisi Mwinjuma almaarufu kama Binamu au Mwana FA, ameamua kutoa albamu yake kwa mashabiki baada ya kukacha hilo kwa miaka miwili kwa kile alichokiita kusambaa kwa wizi wa albamu za wasanii nchini.
Binamu ambaye anawashauri watu wasije mjini huku yeye akiendelea kula bata jijini Dar es Salaam, amesema kwa sasa yupo tayari kuachia albamu hiyo ambayo anadhani itakuwa ni zawadi tosha kwa mashabiki wake.
"Ninatoa albamu kama zawadi kwa mashabiki, kwani ni muda mrefu sijafanya hivyo, ninaamini kuwa nitakapoitoa mashabiki watapata fursa ya kuzisikia nyimbo zangu nyingi ambazo hata hivyo hazijaweza kusikika redioni hata katika televisheni" alisema.
FA ambaye alianza muziki mwaka 1993 aliwahi kupata tuzo kadhaa za muziki na ametamba na singo kama  ‘Alikufa Kwa Ngoma,'Habari Ndiyo Hiyo' na 'Binamu'.

Wednesday, September 14, 2011

"KATIBA MPYA INAHITAJIKA KULETA UFANISI WA KAZI" Maembe...

MSANII wa Muziki wa asili nchini Vitalis Maembe amesema katiba mpya inahitajika ili kuleta ufanisi wa kazi hasa kwa wasanii ambao wanahitaji uhuru katika kazi zao.

Maembe alitoa kauli hiyo alipokuwa akitumbuiza katika jukwaa la sanaa linalofanyika kila siku ya Jumatatu, Baraza la Sanaa la Taifa (Basata).


“Tunahitaji katiba inayoendana na mahitaji ya watanzania katika kuleta chachu ya muziki wa asili, katiba isiyo ya kikoloni itakayoruhusu tume huru na itakayotoa uhuru kwa wasanii kutokana na kile wanachokiimba, ” alisema.

Aidha alisema, muziki wa zamani ulikuwa unatumia katiba kwa asilimia kubwa na ndio maana uliweza kufanikiwa ndani na nje ya nchi.

“Maudhui ya kimuziki ni lazima yaendane na katiba kama ilivyokuwa zamani,katiba lazima imfanye msanii kuwa huru na kuimba kile anachokiamini ilimradi asivunje maadili katika kazi yake ya kimuziki”

Alisema kuwa aina ya muziki wake umejikita zaidi katika kutoa elimu dhidi ya rushwa, uvivu kwa vijana kwa kisasa ili kuweza kuleta madiliko chanya katika maendeleo ya nchi.

Aliongeza kuwa wanamuziki ndio kioo katika jamii yoyote ile dunia, na ndio watu wanaoweza kuleta mabadiliko kutokana na kile wanachokiimba kwa jamii husika.

Hivi sasa Maembe anatamba na nyimbo kama Sumu ya teja, Afrika shilingi tano na nyingine nying.

Tuesday, September 13, 2011

Women entrepreneurs’ forum starts tomorrow


Dar es Salaam. Women entrepreneurs are expected to gather at Dar es Salaam’s Mnazi Mmoja grounds tomorrow and showcase their products.

The forum, organized by Tanzania Women Entrepreneurs Network and Development Exposition (Twende), will run for three days seeks to give a chance for women entrepreneurs to network and develop their businesses, according to the event coordinator, Gloria Mongella (pictured).

The forum will be held alongside a seminar whereby Twende will be equipping women entrepreneurs with skills to prosper in their various areas of concentration.

Community Development, Gender and Children minister, Ms Sophia Simba will officiate the event, which will be held for the second time in Twende’s calendar.

Sunday, September 11, 2011

MATUKIO KATIKA PICHA YA MISS TANZANIA 2011...

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda, Juliana Kinyemuzi akitoa burudani wakati wa kinyang’anyilo cha kumsaka mlimbwende wa Vodacom Miss Tanzania 2011 kilichofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya majaji wakibadilishana mawazo kwenye king’anyilo cha kumsaka mlimbwende wa Vodacom Miss Tanzania 2011 kilichofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam
Pichani ni baadhi ya warembo walioshinda vipaji mbalimbali katika kinyang’anyilo cha kumsaka mlimbwende wa Vodacom Miss Tanzania 2011 kilichofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam juzi.kushoto ni Mwajabu Juma ,Trace Sospeter ,Maria Clara,Rose Hubert na Alexia Williams
Vodacom Miss Tanzania 2010, Genavive Mpagala  (kulia) akimvika taji Miss Vodacom 2011,Salha Israel  aliyekaa baada ya kutangaza mshindi wa kinyang’anyilo cha kumsaka mlimbwende wa Vodacom Miss Tanzania 2011 kilichofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam
Miss Vodacom 2011, Salha Israel akitabasmu huku akiwapungia mikono wageni waalikwa baada ya kutangazwa kutwaa taji hilo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam .Kushoto ni Mrembo aliyeshika nafasi ya Tatu, Alexia William s na Kulia ni Mrembo wa Pili,Tracy Sospeter . 
Voda Miss Vodacom 2011, Salha Israel (katikati) akionesha funguo wa gali aina ya Jeep Baada ya kutwaa taji hilo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam .Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Dietlof Mare

Mwanamuziki Bob Junior akitoa burudani kwenye king’anyilo cha kumsaka mlimbwende wa Vodacom Miss Tanzania 2011 kilichofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam
Mwanamuziki Diamond akiburudisha mashabiki walihudhuria kwenye kinyang’anyilo cha kumsaka mlimbwende wa Vodacom Miss Tanzania 2011

Michael Jackson wa Tanzania Emmanuel Maganga akiwapagawisha mashabiki walihudhuria kwenye kinyang’anyilo cha kumsaka mlimbwende wa Vodacom Miss Tanzania 2011

SALHA AWA MSHINDI WA VODACOM MISS TZ 2011...

Vodacom Miss Tanzania,Sarha Israel (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mshindi wa Pili,Tracy Sospeter (kulia) na mshindi wa tatu,Alexia William mara baada ya kutangazwa usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar. Kwa ushindi huo Sarha Israel anakuwa Vodacom Miss Tanzania 2011-2012 na kunyakua gari aina ya Jeep lenye thamani ya shilinngi milioni 72 lililotolewa na wadhamini wakuu kampuni ya simu za mkononi Vodacom Tanzania na Kampuni ya kuuza magari ya CFAO MOTORS ya jijini Dar es salaam