KUNDI la Muziki wa Injili la Ambassador of Christ kutoka Rwanda limetua na kuahidi kushusha shoo ya nguvu LEO Jumapili kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa albamu yao ya'Dukwie Gushima' ikiwa na maana ya Twapita Kushukuru.
Albamu hiyo ni mpya baada ya ajali iliyoua wasanii watatu wa kundi hilo; Filbert, Ephraem na Amos iliyotokea Kahama, Shinyanga Mei mwaka huu wakati kundi hilo likirudi mjini Kigali baada ya kutoka Dar es Salaam.
Albamu hiyo ina nyimbo 11, lakini watatumbuiza pia kwa nyimbo za 'Kwetu Pazuri', 'Kazi Tufanye' na nyinginezo.
Kundi hilo ambalo limejipatia umaarufu mkubwa hususani ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kutokana na kuimba nyimbo kwakutumia kutumia lugha fasaha ya Kiswahili,lilitua jijini Dar es Salaam jana Ijumaa likiwa na waimbaji 33.
Mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kulakiwa na umati mkubwa wa wapenzi wa muziki huo, mwalimu wa kwaya wa kundi hilo,Sozzy Joram alisema;
Tumeamua kurudi Tanzania kuja kuzindua albam yetu kwavile ni nchi yenye watu wakarimu,tulikuwa pamoja wakati tulipopata ajali na wenzetu watatu wakafariki.
Kitu ninachoweza kuwaahidi ndugu zetu Watanzania waje kwa wingi Jumapili kwa pamoja tumsifu Mungu kwa kutuepusha na ajali mbaya kwavile tungeweza kufa wote,"alisema Joram.