Tuesday, October 12, 2010
Nane waingia fainal, wapata fursa ya kuonyesha kazi zao jukwaa la Swahili Fashion Week 2010.
“Contemporary Swahili” ni kauli mbiu ya shindano 2010
Hatimae majina ya wabunifu 8 wenye vipaji ambao wameingia fainali na kushindania zawadi ya mwaka katika onyesho kubwa la wiki la mavazi Swahili Fashion Week 2010 wapatikana.
Uchaguzi wa wabunifu wa mavazi wanaochipukia umefanyika Septemba 10 katika hotel ya Southern Sun jijini Dar es salaam, ambapo majina 8 yalichaguliwa na jopo la majaji wanne ambao ni Jamila Swai ambae ni mbunifu wa mavazi hapa nchini, Mkurugenzi wa Sanaa Nsao Shalua kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (National arts Council), Michelangelo Adam kutoka ubalozo wa Italia hapa ncini na Mustafa Hassanali.
Wabunifu hao 8 waliongia fainali watashindana katika kuonyesha kazi zao katika onyesho kubwa la wiki la mavazi Swahili Fashion Week litakayofanyika mwezi wa Novemba mwaka huu.
Mratibu wa Swahili Fashion Week, Ndugu Washington Benbella amesema kuwa “ Wabunifu wote 16 walikuwa wazuri na wameonyesha vipaji vya hali ya juu, na kuonyesha kuaTanzania ina vipaji vikubwa katika sanaa ya ubunifu wa mavazi”.
Wabunifu wa mavazi wanaochipukia waliofanikiwa kuingia fainali ni pamoja na Pooja Narendrakumar Jeshang, Abduel Urassa, Shaban Mfaume, Kelvin Boniface, Subira Rahma Wahure, Angelina Muna and Grace Kijo.
Majaji walikuwa na kazi ya ziada, kwani walikuwa makini katika kuangalia mambo mbalimbali ili kuweza kupitisha majina 8 ya wabunifu wa mavazi wanaochipukia, kwani walilazimika kuangalia uwezo katika ubunifu na kuchora, kwa kiasi gani mchoro unavitia, rangi iliyotumika katika mchoro na mambo mbalimbali yanayohusiana na ubunifu kwa ujumla.
Swahili Fashion Week ni jukwaa pekee linalowaleta pamoja wabunifu wa mavazi na watengenezaji wa bidhaa za mapambo kutoka nchi zote zinazozungumza lugha ya Kiswahili, ili kuonyesha ubunifu wao, kuuza bidhaa wanazozalisha, kubuni ajira, sambamba na kutengeneza mtandao kwa wabunifu kutoka maoneo hayo wanayoongea lugha ya Kiswahili, sambamba na kuhimiza dhana nzima ya kuthamini bidhaa zinazotengenezwa Afrika Mshariki.
Msisitizo zaidi umewekwa katika kuhakikisha kwamba sekta ya ubunifu inakuwa kikanda. Swahili Fashion Week inalenga kukuza sanaa ya ubunifu na kuwa jukwaa bora la kibiashara kimataifa kwa nchi za Afrika Mahariki.
Kwa mara ya tatu sasa Swahili Fashion Week imekuwa ikifanyika, ambapo kwa mwaka huu itafanyika November 2010, Dar Es Salaam , Tanzania .
Shindano hili linafanyika kwa mwaka wa tatu sasa, halina kikwazo cha umri, na linatoa fursa kwa watu wote wanaoamini kwamba wana kipaji cha ubunifu, na wanataka kuwa wabunifu. “Swahili Fashion Week ni jukwaa bora kwa wabunifu kuonyesha uwezo wao wa ubunifu na kuibua sindano la wabunifu wapya, ni jukwaa linalowawezesha watu kufikia malengo yao ”, aliongeza Mustafa Hassanali muandaaji wa Swahili Fashion Week.
Posted by thazealot at 10:55 AM 0 comments
Saturday, October 9, 2010
Historia fupi ya consolata Lukosi na ndoto zake za kuwa mfanyabiashara wa kimataifa.
Jina lake halisi ni Consolata Lukosi,Ana umri wa miaka 20,anakotoka ni manispaa ya Ilala,Kabila lake Mhehe Consolata ni mtoto wa kwanza kati ya watoto watatu katika familia ya Bwana na Bi. Lukosi. alizaliwa mpanda mkoa wa Rukwa na baadaye kuhamia Mbeya na kujiunga shule ya msingi ya Isanga. Elimu ya sekondari ameisoma Mbeya Secondary School , kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne. Baada ya hapo alihamia Dar es Salaam na kujiunga na Shule ya Sekondari ya Jitegemee, aliposoma kidato cha tano na cha sita.
Consolata anasema fani ya urembo ni fani ambayo alikuwa anaipenda sana tangu utotoni na pia ilikuwa ni kati ya malengo aliyodhamiria kufanikisha. Alianza kufanya mambo ya urembo kupitia kitongoji cha Tabata aliposhiriki na kushinda Miss Tabata 2010. Baada ya hapo alifanikiwa kuingia kambi ya Miss Ilala kuwania taji hilo , ambapo alifanikiwa kushika nafasi ya tatu .
Consolata angependa kuwa mfanyabiashara wa kimataifa aliye na kampuni yake binafsi na vilevile kuendelea kujihusisha na fani ya urembo hasa kupitia, uwanamitindo. Hivi punde atajiunga na chuo cha Learn It ambapo atachukua kozi ya biashara itakayomuwezesha kufanikisha lengo lake la kuwa na kampuni na kuwa mfanya biashara bora.
Akizungumzia kazi anazo fanya na kampuni ya bia ya TBL kupitia kinywaji cha REDDS Consolata ameanza kwa kusema ana furaha kubwa sana kuwa na bahati ya kuwa balozi wa Kinywaji cha Redds kwa mwaka wa 2010. "Ninapokea kazi nzuri ya yenye heshima walizofanya wenzangu Victoria , Jokate na Natalia. Walikuwa ni mabalozi wazuri sana na kupitia ushauri na uongozi wao natarajia kufanya kazi itakayoleta mabadiliko kwangu na kwa jamii yangu na pia kwa Redds na kampuni ya Tbl" asema Consolata.
Anatazamia kufanya kazi kwa ukaribu sana na jamii hasa kupitia shughuli za kampuni mama ya kinywaji cha Redds, ambayo inatarajia kuanzisha miradi mbalimbali ya maji nchini na vilevile kwa kuwa kinywaji cha Redds kinajihusisha moja kwa moja na kuimarisha sekta ya ubunifu na mitindo anasema atakuwa mstari wa mbele katika shughuli zitakazoihusiana na uimarishaji huu. Vilevile anatarajia pia binafsi kuisaidia jamii yake kwa kupigania haki za wanawake na watoto pamoja na kuielimisha jamii kuhusu kujiepusha na majanga kama Ukimwi na namna ya kujiepusha nayo.
Consolata anachowambia ma miss ni kuwa angependa wajue kuwa yahitaji sana moyo kuwa katika fani hii hivyo wasikate tama na kwa wale ambao hawakufanikiwa kufikia ngazi ya taifa wasisite kujaribu tena na pia waendelee kusoma na kujiendeleza katika shughuli za kuwaletea maendeleo wao na jamii inayowazunguka..
kwa sasa Consolata anaishi YomboVituka na Dada yake.
Posted by thazealot at 1:39 PM 0 comments
Sunday, October 3, 2010
Hii ndiyo ajali iliyoangamiza zaidi ya watu 230 DRC baada ya gari la mafuta kupinduka.,kama unapresha usiangalie
Posted by thazealot at 1:49 PM 0 comments
Friday, October 1, 2010
"The Sporah Show " mbadala wa show ya oprah hapa bongo.
Tumezoea kuwaona watangazaji na waendesha vipindi vya televisheni maarufu kama vile Oprah Winfrey na kipindi chake Oprah Winfrey Show na Tyra Banks na kipindi chake The Tyra Banks Show wote hawa wakiwa ni wanawake wa Kiafrika wenye asili ya Marekani waliofanikiwa na kujizolea umaarufu kutokana na vipindi vyao hivyo.
Pamoja na kuwa ni Wamarekani weusi, lakini bado tukiwa kama Watanzania hatuwezi kujitapa ama kujivunia sana pamoja kwamba kwa asili wana damu ya Kiafrika.
Sporah akiwa na alikiba pamoja na Mims.
Lakini sasa huenda umefika wakati wetu nasi kujivunia watu wetu, watangazaji wetu, Watanzania wenzetu ambao wameamua kuvunja ukuta na kujitosa katika uendeshaji wa vipindi ama maonesho ya televisheni kama ilivyo kwa Oprah na Tyra.
Tuna kila sababu sasa kama watanzania kujivunia kwa sababu tumepata Mtanzania mwenzetu ambaye ameamua kuendesha kipindi cha mazungumzo katika televisheni, na huyu si mwingine bali ni Irene Sporah Njau ambaye ameanzisha Kipindi cha Majadiliano cha Kiafrika kinachojulikana kama The Sporah Show akiwa nchini Uingereza.
Irene Sporah Njau.
Kama hiyo haitoshi, binti huyo kutoka Tanzania ambaye hujulikana zaidi kwa jina la Sporah kuanzia Juni 11 The Sporah Show itakuwa ikioneshwa hapa nyumbani kupitia kituo kimojawapo cha televisheni nchini katika siku za Ijumaa na Jumamosi
"Kwa kweli TV Show ilikuwa ni ndoto yangu, ila nilipofika Uingereza na kuona jinsi ambavyo nchi za wenzetu zina mifumo tofauti ya kuelimisha jamii, nilijikuta vikinipa motisha zaidi ya kutaka kutimiza ndoto yangu ndipo nilipopata wazo la kuanzisha kipindi cha The Sporah Show" asema Irene Sporah Njau.
Posted by thazealot at 2:40 PM 0 comments
Usiku wa Kanga kufanyika leo usiku
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Chiku Galawa, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ‘Usiku wa Kanga za Kale’ utakaofanyika Oktoba mosi kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Fabak Fashion, Asia Idarous, tamasha hilo litashirikisha wabunifu wa mavazi na wadau mbalimbali, wakiwemo kina mama na kina baba watakaopanda jukwaani kuonyesha mavazi ya kanga na vionjo.
Idarous alisema tamasha hilo litasindikizwa na burudani kutoka kundi la Jahazi Modern Taarab, waimbaji nyota Khadija Kopa, Rukia Ramadhani, Sabah Salum Muchacho na Baby Madaha.
Aidha, Idarous alitaja viingilio katika usiku huo kuwa ni shilingi 20,000 kwa viti maalumu ‘VIP’ na shilingi 10,000 kwa viti vya kawaida, ambako tiketi zinapatikana Fabak Fashions.
usiku huo wa kanga wataoonesha mavazi ni macelebrity wa bongo wakiwemo waigizaji wa filamu, wadau wa mitindo na watu kadhaa wanaofahamikatika sekta tofauti tofauti
Posted by thazealot at 2:17 PM 0 comments
Sunday, September 26, 2010
'East African Bash' yawakutanisha AY Amani na Ngoni ndani ya Da’ West.
Wasanii Ambwene Yesaya `AY`’ kutoka Tanzania, Ngoni kutoka Uganda na Amani wa Kenya, wanatarajiwa kuonyeshana kazi jijini Dar es Salaam kesho katika tamasha maalum la muziki lililopewa jina la 'East African Bash' na kushirikisha nyota wa nchi hizo wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashairiki.
![]() |
AY na wakali wenzake hao, watachuana kwenye ukumbi wa Da’ West uliopo Tabata na baada ya hapo, watachuana tena katika onyesho la pamoja litakalofanyika siku moja baadaye kwenye eneo la ufukwe wa Mbalamwezi jijini Dar.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, AY ambaye ni mmoja wa washiriki, alisema amejipanga kuwawakilisha vyema Watanzania kwa kuonyesha kiwango cha juu na kuwaduwaza wanamuziki kutoka Kenya na Uganda.
"Najua hili ni tamasha kubwa na mimi ndiye niliyebahatika kuwa mwakilishi pekee wa Tanzania… kwa sababu hiyo, nataka kufanya kweli ili kuwakilisha vyema," alisema AY.
Kwa upande wake mratibu wa tamasha hilo, Dennis Busulwa, alisema kuwa lengo kubwa la tamasha hilo ni kuendeleza umoja wa wanamuziki wa nchi za Afrika Mashariki.
Posted by thazealot at 7:58 PM 0 comments
Saturday, September 25, 2010
MWISHO AMVISHA PETE MERYL WA BBA JUMUMAMOSI HII.
Jioni ya leo tarehe 25 september Mshiriki wa BBA all stars kutoka Tanzania Mwisho Mwapamba ameweka historia ndani ya jumba hilo kwa kumchumbia mshiriki mwenzake aitwaye Meryl kutoka Namibia,
Mwisho alimvisha pete yenye madini ya Tanzanite mchumba wake Meryl huku tendo hilo likishuhudiwa na Baba yake mzazi na Meryl pamoja na shangazi yake, wakati huo kwa upande wa mwisho alikuwepo kaka yake aitwaye Roberty Mwapamba ambaye aliiwakisha familia yao.
Mwisho na maryl ndani ya BBA all Stars.
Posted by thazealot at 2:46 PM 0 comments
Tuesday, September 21, 2010
MWISHO KUMUOA MERYL WA BBA JMUMAMOSI HII.
Leo Mwisho amekili kwa Big Brother kuwa anatarajia kumuoa Meryl siku ya jmosi 25 September.
katika shughuli zake za kila siku, Big Brother alimuhoji jinsi gani alivyo serious na mpango wake na mwisho alisema.
“Niko serious katika maisha na hivyo haita ni surprise mimi na haita kuwa surprise pia kwa familia yangu na rafiki zangu pia,” Mwisho alisema serious kutoka moyoni.
aliongeza kuwa, atakuwa makini zaidi. Big Brother alimuhoji nani atakuwa ni bestman wake na akasema kuwa atakuwa Uti.
ingawa Uti na Mwisho hawajazungumza kwa takribani siku tatu,lakini Mwisho alisisitiza kuwa Uti atafanya hivyo.
Pale Big Brother alimuhoji kama aliwahi kuzungumza na mmoja wa housemates wa BBA, alijibu “wote” na akasema hakuna kati yao aliyepinga wazo.
Ndani ya siku hii ya leo pia baada ya Mwisho na Mryl kutangaza kutaka kufunga ndoa,Meryl na Mwisho walikuwa wakilumbana kutokana na kile Mwisho anachokisema Maryl anatumia muda mwingi kuwa na housemate wa kiume ndani ya mjengo.
Meryl alijitetea kuwa hana cha kujiepusha bali ni kushirikiana nao hao housemates wenzake wa kiume kwa kuwa yeye ni Mwanamke peke yake aliyebaki mjengoni.
Meryl alijitetea kuwa hana cha kujiepusha bali ni kushirikiana nao hao housemates wenzake wa kiume kwa kuwa yeye ni Mwanamke peke yake aliyebaki mjengoni.
Pamoja na story hiyo mwisho hivi karibuni baada ya kuwa nomionated ktk top five alijimwaga ktk jacuzi na mchumba wake kufurahia..

After the Nominations show, washindi walioingia Top five wakatupia nguo kuleeeee then shaap dip in the jacuzzi. Bro Mwisho na shem wa Tanzania (Meryl) walipiga bonge bonge moja la deeeeep KISS almost four minutes .... daaaaaah ilikuwa utata pale kati mzeee!!!!.
Wadau tufanye uzalendo Bro wetu arudi home na kitita cha madollar kwa kumuokoa kutoka mjengoni by voting thru www.mnetafrica.com/bigbrother then utakuta maelekezo how to vote or thru ur mobile phone.
VOTE 4 MWISHO VOTE 4 TANZANIA.......!!!!!!!!!!!!!!!!
Posted by thazealot at 11:45 AM 0 comments
Thursday, September 16, 2010
DIPLOMA WA TSJ WASHEREKEA BASH NA KILIO CHA MABAO 3 KUTOKA ACC KWENYE MECHI YA KIRAFIKI.
Timu ya Wanafunzi wa Diploma Tsj.
WANAFUNZI Chuo cha uandishi wa habari cha Time school of journalism(TSJ), jana walikuwa na mechi ya kirafiki ya mpira wa miguu baina ya wanafunzi wa A-stashahada (certificate) na Diploma (stashahada) na wanafunzi wa Certificate waliibuka washindi kwa kuwafunga Diploma kwa mabao 3 kwa 2 kwenye mechi hiyo iliyochezwa uwanja wa garden maeneo ya Ilala Bungoni jijini Dar es salaam.
Timu ya Wanafunzi wa ACC TSJ
Wakizungumza na blog hii baadhi ya wachezaji walisema kuwa mechi hiyo ilikuwa ya kirafiki na imejenga umoja na muendelezo wa mazoezi kwa chuo chao kutokana na utani wa jadi uliokuweko baina ya wanafunzi hao ambao wanasomea kozi ya uandishi wa habari katika ngazi tofauti ikiwa ni Certificate na Diploma.
Hata hivyo waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi ya chuo hicho (TISJOSO) ameongeza kuwa mechi hiyo ilifanyika kwa amani bila ya kuwa na ugomvi na malumbano ya hapa na pale na pia akawasititiza wanafunzi kuendelea na moyo huo huo wa kujijenga kimichezo ili waweze kucheza mechi tofauti tofauti na vyuo vingine.
Wakiwa uwanjani.
MBALI na hilo pia chuo cha Time School of Journalism (TSJ) kupitia serikali ya wanafunzi ya chuo hicho wameandaa BASH ya kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa ngazi hizo mbili za certificate na Diploma inayotarajiwa kufanyika katika viwanja vya Cine Club siku ya Jmosi tarehe 18 mwezi wa 9/ 2010.
Kulia ni Miss Tsj Lilian Andrew na Katika ni Benadina Mwita miss no 2 na kushoto ni Somoe Nkomoe mwanafunzi TSJ.
Na akizungumzia maandalizi ya sherehe hiyo waziri wa michezo wa chuo hicho amesema kuwa itakuwa ni bash ya kihistoria na ina muchezo lukuki itakayofanyika hivyo amewasihi wanafunzi kujitokeza katika bash hiyo ili kujifunza na pia kujenga mahusiano mazuri na wanafunzi wenzao wapya. michezo ambayo itakuwepo katika Bash hiyo ni Miss na Mr TSJ, Vichekesho, Maigizo, Kuimba, Kukimbia na gunia, mashindano ya kunywa soda na michezo mingine mingi, na pia amewaaalifu kuwa mgeni rasmi wa shughuli hiyo ni Mhesimiwa IDD AZAR ZUNGU mbunge wa jimbo la Ilala na wageni wengi waalikwa.
Thazealottz inawatakia sherehe njema wanafunzi wa chuo cha TSJ na washerekee kwa amani na maadili.
Posted by thazealot at 5:32 PM 0 comments
Sunday, September 12, 2010
Mambo manne ya kuzingatia Kama unataka kuacha/kupunguza pombe!
Pombe ni burudani, huondoa uchovu na kuchangamsha mwili, lakini wakati mwingine pombe ikimzidi mtu huweza kumharibia hata mipango mbalimbali ya maisha yake. Hapo sasa ndipo shauku ya mtu kutaka kuacha pombe inakuja.
Hata hivyo, pamoja na shauku hiyo ya kuacha pombe, wengi hushindwa kutokana na mwili wake kuwa tayari umeshazoea pombe. Hapa nitakupa njia za kitaalamu kabisa ambazo ikiwa utazitumia kwa umakini, inaweza kuwa rahisi sana kwako wewe mlevi kupunguza kama siyo kuacha kabisa kunywa pombe.
Sasa soma mtiririko ufuatao.
KIMBIA KAMPANI ZA POMBE
Hii ni hatua ya kwanza kabisa ambayo unatakiwa kuifanya wewe ambaye una nia ya kupunguza au kuacha kabisa kunywa pombe. Achana na marafiki zako walevi, usipende kufanya vikao katika baa au kumbi za starehe.
TAFUTA VITU VYA KUFANYA
Wahi kufika nyumbani, na tafuta vitu vingine vya kufanya kama kusoma magazeti, kuangalia filamu na mengine mengi ya kupendeza. Ni rahisi tu kufanya hivyo. Kwanza uanweza ukabadilisha ratiba yako ya kazini. Jiongezee ubize kwa kadri uwezavyo, ili utakavyotoka kazini uwe mchovu, unayewaza maji ya kuoga na kupumzika huku ukipata burudani nyingine kama nilivyoeleza hapo juu.
Wahi kufika nyumbani, na tafuta vitu vingine vya kufanya kama kusoma magazeti, kuangalia filamu na mengine mengi ya kupendeza. Ni rahisi tu kufanya hivyo. Kwanza uanweza ukabadilisha ratiba yako ya kazini. Jiongezee ubize kwa kadri uwezavyo, ili utakavyotoka kazini uwe mchovu, unayewaza maji ya kuoga na kupumzika huku ukipata burudani nyingine kama nilivyoeleza hapo juu.
BADILI VINYWAJI
Kwakweli ni vigumu sana kuacha pombe, lakini kama una nia ni rahisi pia. Pindi uhisipo hamu ya kunywa pombe, tumia muda huo kunywa chai, kahawa, juisi au maziwa. Kwa kawaida, baada ya kunywa vinywaji vya baridi au moto vyenye sukari, hukata au kupunguza hamu ya kunywa pombe.
AMUA KWA DHATI
Pamoja na yote hayo niliyoyafafanua hapo juu, ni jukumu lako wewe na moyo wako kuamua kwa dhati kabisa kwamba “SASA HUTAKI TENA KUNYWA POMBE! Ikiwa utakuwa na imani hii moyoni mwako, ni rahisi sana kuacha pombe.
Posted by thazealot at 6:30 PM 0 comments
Subscribe to:
Posts (Atom)


























