BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS »

www.thazealottz.blogspot.com

Promo

Monday, December 27, 2010

THIS BLOG IS UNDER CONSTRUCTION.


WADAU WANGU NIKO KATIKA MABORESHO YA BLOG HII HIVYO NINAOMBA RADHI KUWA SITAWAHABARISHA KWA MUDA KIDOGO KATIKA KUWEKA MAMBO SAWA KUPITIA BLOG HII LAKINI SOON JANUARY HALI ITAKUWA KAMA KAWAIDA..

nawatakia heri ya mwaka mpya 2011.


"NAITWA FRANK AMAN MAWENYA NI BLOGGER NAYEJIHUSISHA NA HABARI ZA BURUDANI KUPITIA BLOG ZANGU ZA filamutanzania.blogspot.com NA thazealottz.blogspot.com.NATOA SHUKRANI ZANGU ZA PEKEE ZIENDE KWAKO WEWE MDAU WANGU WA HABARI KUPITIA BLOG ZANGU AMBAZO NI MAHUSUSI KATIKA KUKUPASHA HABARI ZA KI-ENTERTAINMENT KWA HAPA BONGO NA NJE YA BONGO.NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU KWA MUNGU MUUMBA WETU AMBAYE AMENIWEKA NA AMEKUWEKA HAI MPAKA SASA TUNAELEKEA KUHITIMISHA MWAKA HUU 2010 NA KUKARIBISHA MWAKA MPYA 2011.NAWAPA POLE WADAU WALIOPATWA NA MATATIZO MBALIMBALI YA KIJAMII KAMA MAGONJWA,MISIBA,AJALI NA MATUKIO MENGINE YOTE YA KUHUZUNISHA NA PIA MUNGU AZIWEKE MAHALI PEMA PEPONI ROHO ZA WENZETU WALIOTUTANGULIA MBELE ZA HAKI....

MWAKA 2010 UMEKUWA MWAKA WA MAFANIKIO KWANGU NAMSHUKURU MUNGU KWA HILO LAKINI PIA NAWASHUKURU WATU WALIO NISAPOTI MPAKA HAPA,NA WALIONISAIDIA KWA USHAURI NA MAMBO MENINE MENGI.NAKUAHIDI MAMBO MAKUBWA KWA MWAKA UJAO WA 2011 KWANI KWA SASA NAOMBA KUWAARIFU KUWA BLOG HII ITAKUWA UNDER CONSTRUCTION KWA MUDA ILI KUWEZA KUJA UPYA NA MAMBO MAZURI KABISA HIVYO NAOMBA LADHI KWA WADAU WANGU KWA UKIMYA UTAKAOKUWEPO MPAKA PALE NTAKAPO REJEA JANUARY 2011.NAKUSHUKURU KWA KUWA PAMOJA MWAKA HUU UNAOISHA NA PIA NAKUSIHI ENDELEA KUWA NA MIMI MWANZO MWISHO KWA HABARI KEM KEM ZA KI BURUDANI NDANI NA NJE" KUTAKUWA NA MABADILIKO MENGI SEGMENT MPYA MWONEKANO MPYA WA BLOG NA HABARI NZURI NA HOTTEST/LATEST KWAKO KUZIPATA.

WAWEZA KUWASILIANA NA MIMI KWA MAONI ZAIDI NA USHAURI KUPITIA E MAIL ADDRESS YANGU famanmawenya@yahoo.fr AMA WAWEZA KUTANA NA MIMI KATIKA FACEBOOK KWA JINA LA FRANK THA ZEALOT AMA ANDIKA fzealot/facebook UTANIPATA KWA STORY ZAIDI.

Thursday, December 23, 2010

MR. CHOCOLATE FLAVA.. ON BOXING DAY NDANI YA BONGO STARZ NITE CLUB BILLICANAZ.


CLUB BILICANAZ inakuletea show kali ya Kuufunga mwaka 2010 BOXING DAY Jumapili hii ya tarehe 26 Dec 2010. Watakuwepo vijana Watanashati kutoka SHAROBARO CREW wakiongozwa na PRESIDENT MR. CHOCOLATE a.k.a. BOB JUNIOR na wakisindikizwa na SUPA DJz a.k.a. MTU TATU. DJ EBRAH, DJ EJAY NA DJ MARIO kwa kiingilio cha BUKU TANO TU. Ni Jumapili hii ndani ya BONGO STARZ NITE CLUB BILICANAZ usikose...

Tuesday, December 21, 2010

NIAJE.COM CHRISTMAS BEACH PARTY IN MOMBASA.


Niaje.com gives you a treat of the year, we are hosting the biggest beach party of 2010 on this year’s Christmas eve! Branded the Niaje Christmas Beach Party, we are giving Kenyans and visitors a first time performance of Wahu and her husband Nameless on the same stage doing their popular hits and a duet Christmas Carol.The show will also feature on of Tanzania’s greatest vocalist and recording artiste, T.I.D. live on stage.

Nameless (David Mathenge) is undoubtedly Kenya’s biggest sensation in music and one of the most consistent musicians Kenya has. He is also an award winning artiste who has attained international recognition and also is attributed as one of the pioneers of what is today’s Kenyan music.

Wahu Kagwi is married to Nameless and for a unique first time, they will be performing together on a single stage. Christmas cant come better.

T.I.D. will also be performing his hits including zeze, siamini among many others.

Gate charge will be 500 shillings for normal tickets and an extra 500 shillings for VIP area and VIP bar access.

This will be held at the Big Tree Beach Bar in Bamburi Beach, Mombasa.

Other’s at the show will be Niaje’s DJ Raidar, DJ Hassan of the HomeBoyz, DJ Bonnz among others.

Monday, December 20, 2010

STEP UP PLAYER PRESENTS BALLERZ AND DIVAS BEACH PARTY

Friday, December 17, 2010

MSHINDI WA BONGO STAR SEARCH 4 NI MARIAM MOHAMED


MSHIRIKI wa shindano la kusaka vipaji vya uimbaji la Bongo Star Search,MIRIAM MOHAMED mwenye namba ya ushiriki BSS 17 Ameibuka mshindi kwa kujinyakulia kiasi cha shilingi milioni 30 kutoka kwa wadhamini wakuu wa Shindano hilo ambao ni TBL kupitia kinywaji cha Kilimanjaro Premium Lager.
 
Mariam Mohamed.


Mshindi wa pili wa shindano hilo ni... James Martin BSS 14 ....ambaye amejinyakulia kitita cha shilingi milioni kumi kutoka kwa wadhamini wenza wa shindano hilo ambao ni Airtel.
 
 James Martin.

Na mshindi wa tatu ni... joseph Payne BSS 07....ambaye amejinyakulia kiasi cha shilingi milioni tano 
joseph Payne.
Wakifuatiwa na Bella Kombo. ambaye ni mshindi wa nne na Waziri Salum ambaye ni mshiriki namba BSS 11 ambaye ni mshindi wa tano wa shindano hilo
Bella Kombo.
 
Waziri Salum. 

Wednesday, December 15, 2010

MARLAW,CHEGE KUTUMBUIZA BSS IJUMAA.



NYOTA kadhaa wa muziki wa kizazi kipya wakiwemo Marlaw, Diamond, Chege na Mh Temba watatumbuiza katika fainali ya kumsaka kinara wa shindano la ‘Kilimanjaro Bongo Star Search 2010’ kwenye ukumbi wa Mlimani city jijini Dar Es Salaam ijumaa.

 Ritha Paulsen na Meneja wa TBL.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam jana, mkurugrnzi  wa kampuni ya Benchmark Production inayoandaa shindano hilo, Ritha Paulsen, aliwataja nyota wengine watakao tumbuiza siku hiyo kuwa ni Mwasiti, Joh makini, Imani na Cindy kutoka nchini Uganda.
Alisema kuwa fainali hizo zitaoneshwa na moja kwa moja na kituo cha televisheni cha ITV kuanzia saa 1:00 usiku na maandalizi yote yamekamilika.
Nyota watano walioingia fainali na kuwania zawadi ya Kwanza ya  kitita cha Sh. Milioni 30 ni Bella Kombo mwenye namba BSS 02, joseph Payne BSS 07, Mariam Mohamed BSS 17, James Martin BSS 14 na Waziri Salum ambaye ni mshiriki namba BSS 11.
 Washiriki wakionesha zawadi ya mshindi wa kwanza.

Mshindi wa pili atapata Sh. Milioni 10 huku watatu akitarajiwa kuzoa Sh. Milioni tano.
Ritha alisema zawadi ya kwanza imetolewa na wadhamini wakuu wa shindano hilo, kampuni ya bia ya TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro, wakati zawadi ya mshindi wa pili imetolewa na kampuni ya huduma ya simu za mkononi ya Airtel.
 Tano bora ya BSS 2010.

Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George kavishe, alisema kuwa kampuni yake imeungana na Benchmark katika shindano hilo kwa nia ya kuibua vipaji vya muziki wa Tanzania.
Bella Kombo na joseph Payne  

Monday, December 13, 2010

FAINALI YA BSS 2010 KUFANYIKA IJUMAA.


HATIMAYE washiriki watano wameingia fainali za shindano la Bongo star search na watachuana kumtafuta mshindi katika fainali itakayofanyika Ijumaa kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar Es Salaam.
Washiriki hao wameingia katika hatua hiyo baada ya washiriki wenzao watatu kutangazwa kuaga shindano hilo jana wakati walipofanya 'shoo' kwenye ukumbi wa Water front na kurushwa na kitua cha televisheni cha ITV.
Shoo hiyo ilipambwa na wasanii nyota kadhaa wakiwemo Banana Zoro, Mwasiti, Tundaman, Maunda zoro, Amini, Barnaba, Marlaw na Patricia hilal, amabo waliimba pamoja na washiriki wa BSS.

Washiriki watano walioingia katika fainali hiyo baada ya kupigiwa kura nyingi kutoka kwa wananchi ni Waziri salum, Bella Kombo, James Martin, Joseph Payne na Mariam Mohamed.
Washiriki watatu walioaga michuano baada ya kupata kura chache ni Christabella nzowa, Haji Ramadhani na Chiby Dayo.
Mshindi wa BSS mwaka huu atajinyakulia zawadi ya shilingi milioni 30.

DK REMMY ONGALA AFARIKI DUNIA.


Habari za kusikitisha zilizofikia leo asubuhi hii ni kwamba msanii maarufu hapa Tanzania mwenye asili ya kiZaire, Dr. Remmy Ongala, amefariki dunia.
Inasadikika kwamba Ongala alipelekwa hospitali kuu ya Muhimbili jijini Dar es salaam baada ya kuzidiwa usiku wa Jumapili. Alitangazwa marehemu mapema Jumatatu baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya na madaktari kushindwa kumsaidia.
Remmy Ongala atakumbukwa zaidi kwa ustadi wake kwa kupiga guitar na uimbaji wake ambao uliweza kuzivuta hisia za wengi kwa miaka 30 aliyokuwa akishughulika na muziki.
Tunaiombea familia ya Dr. Ongala faraja na Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Fally Ipupa na 2Face Vinara Tuzo za Mama MTV.


Wasanii Fally Ipupa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pamoja na 2face Idibia wa Nigeria Jana usiku wameibuka vinara wa tuzo za MaMa’z kwa mwaka 2010 baada ya kujinyakulia jumla ya tuzo mbili kila mmoja.
Wasanii hao walikuwa wanawania tuzo zaidi ya tatu katika vipengele tofauti na baadaye kujinyakulia tuzo za Video bora. Msanii bora wa Francophone ilienda kwa Fally Ipupa wakati  2Face akibeba Msanii wa mwaka na msanii bora wa kiume.

Sherehe hizo za kuwatuza wasanii wa kiafrika zilianza mida ya saa moja jioni ambapo wasanii mbali mbali pamoja na wageni waalikwa waliwasili katika eneo la Red Carpet kabla ya kupiga picha na kujipatia vinywaji vilivyokuwa tayari kabisa kwa ajili ya wageni hao.
Msanii wa Tanzania Diamond aliondoka mikono mitupu licha ya kupata nafasi ya kuimba pamoja na P-Unit na Teargas katika jukwaa moja.

Aidha sherehe hiyo zilianza rasmi majira ya saa tatu na nusu ambako msanii kutoka Marekani Rick Ross alikuwa wa kwanza kupanda jukwaani na kuamsha nderemo, vifijo na kelele za kutosha ukumbi mzima kabla ya kutoa fursa kwa tuzo ya kwanza kabisa kutolewa ambayo ilikuwa video bora iliyokwenda kwa Fally Ipupa.
Wasanii wengine waliopiga shoo ni pamoja na Moze Radio na Weasle, Jozi, Big Nuz, Sasha, Cabo Snoop, Barbara Kanam, Fally Ipupa, J Martins, 2 Face, Wande Coal, T-Pain, Mo Cheddah  na Eve.

Baadhi ya watu maarufu waliokuwemo katika tuzo hizo ni pamoja na mchezaji wa mpira J J Okocha, Tatiana Durao, Munya na mmiliki wa kituo hicho cha televisheni cha MTV, Bw. Tedd Turner.

Sherehe hizo za kutuza wasanii wa kiafrika za MAMAs zimeletwa kwenu kwa udhamini wa Airtel, Master Card, Halmashauri ya Jiji la Lagos pamoja na hoteli ya nyota tano Eko Suites ambako ukumbi wake wa Eko Center ulitumika.

Friday, December 10, 2010

STEP UP PREYER BEACH PARTY.

Bonge la party litakalo fanyika pande za mbalamwezi Beach club Mikocheni siku ya alhamisi tarehe 23 december 2010. Show hii iko powered na Clouds TV kupitia kipindi cha step up prayaz... Bata za beach party utazipata kwa buku 5 au buku 7 mlangoni.

Wednesday, December 8, 2010

PETER MSECHU AWASILI NYUMBANI-TZ

peter msuchu akirajea nchini.

 moja ya shamla shamla za kumpokea.
fuuull happy being back home..

 wecome back peter.


Akiwa katika pozi home..

Karibu sana msechu kutokja huko kenya katika mashindano ya Tusker project fame ki ukweli umetuwakilisha vizuri Tanzania tunaamini umefungua njia kwa watanzania wengine kufanya vizuri katika mashindano hayo kwa session zinazofuata..  tha zealot

Monday, December 6, 2010

AMPLIFIER SHOW MPYA KUTOKA KWA MILLARD AYO CLOUDS FM.


LEO katika pita pita zangu katika kusikiliza Radio za hapa kwetu TZ nimepata nafasi ku tune katika 88.4 Clouds Fm peoples station mida ya saa moja hivi na nimepata kusikia sauti ya mtangazaji ambaye nilikuwa nimemiss kwa muda sauti yake, anafahamika kama MILLARD AYO  aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha Radio cha Radio 1 stereo hivi sasa ni mwajiriwa  mtangazaji wa kituo cha  radio cha Clouds fm na leo alikuwa katika show yake mpya ya AMPLIFIER ambayo imeshika nafasi ya kipindi cha BAMBATAA kilichokuwa kikiongozzwa na mwanadada Sofia Kessy hivi sasa hakitakuwepo tena na badala yake wapenzi wa station hii tutapata nafasi ya kusilia kipindi hiki cha Millard kila siku za wiki kuanzia saa moja mpaka saa tatu usiku j3 hadi ijumaa.



Kijana huyu amekuja kivingine kabisa na show yake ni bonge la show zaidi ya ile aliyokuwa nayo Radio nayo ya Milzo 101.Pia kuanzia January 2011 atakuwa na show yake mpya kupitia kitua cha televisinon cha Clouds TV.

Sunday, December 5, 2010

DAVIS NTARE AJISHINDIA MIL.5 KSHS TUSKER PROJECT FAME 4.

Mshiriki DAVIS HILLARY NTARE aliyeshiriki mashindano ya kuibua vipaji vya uimbaji hapa Afrika ya mashariki na kati la TUSKER PROJECT FAME, ameibuka mshindi katika kinyang'anyiro hicho ambacho kinahusisha nchi sita kutoka Afrika Mashariki. Davis amejinyakulia kiasi cha shilingi milioni 5 za kenya. 

Hii ni mara ya pili kwa nchi ya Uganda kunyakua ushindi huo, kwa mara ya kwanza katika Tusker Project Fame season 2 ushindi ulichukuliwa na Esther Nabaasa, na PTF3 ushindi ulikwenda kwa Alpha kutoka nchini Rwanda ambaye pia aliibuka tena mshindi katika tuzo za PAM akiwa kama PAM best artiste from Rwanda.

TANZANIA ikiwa kama washiriki katika shindano hilo imeweza kushika nafasi ya pili ikiwakilishwa na PETER MSECHU, nafasi ya tatu imeshikwa na STEVEN kutoka Kenya na nafasi ya nne ikiwa imeshikwa na AMILEENa kutoka Kenya pia.
Nampongeza sana Devis kwa ushindi huo, pia Msechu kwa kuweza kufika nafasi hiyo kubwa ambayo Tanzania hatujawahi ifika kwa mashindano hayo, pia nampongeza kwa kuweza kuiwakilisha Tanzania ipasavyo, bila kuwasau washiriki wengine kutoka Tanzania, Leah Moud, Aneth,na Cynthia ki ukweli wamejitahidi sana.

Changamoto kwa watanzania wenzangu jamani tushiriki kikamilifu katika kuwasappoti wenzetu wanapokuwa katika mashindano hayo ili na sisi siku moja tuweze kunyakua ushindi huo. Tujitolee kuwapigia kura washiriki kwa kila tuwezavyo kwani kilichomwangusha Msechu ni kura na sio suala la uimbaji..

Friday, November 26, 2010

Ujio Mpya Wa Tough Records



Ujio Mpya Wa Tough RecordsHii ni Studio ambayo ilishawahi kuwepo hapo miaka ya nyuma chini ya producer Mona G.But kutokana na mambo flani flani ya kimaisha ilisitishwa kwa muda.Lakini sasa Imerudi Tena Kwa Kishindo 

Chini Ya Producer mdogo Aliyejawa Skillz Za kutosha Kuweza Kuipeleka Game Ya Bongo Overseas Anayekwenda kwa jina la YOUN` GQ.So Let Do The Sheetz In Reality Katika NEW TOUGH RECORDsPamoja!!!!!!!!!!!!! 

Na kwa sasa inapiga dili zake Moro town(MASIKA)\
Kwa Mawasiliano zaidi +255712222244

Thursday, November 25, 2010

WATANZANIA TUSHIRIKI KUMPIGIA KURA PETER MSECHU ABAKI KATIKA TUSKER PROJECT FAME SEASON 4


 Peter Msechu
HII ni season ya nne tangu shindano la kusaka vipaji vya uimbaji la TUSKER PROJECT FAME lianzishwe na kampuni ya bia ya EAST AFRICA BREWELIES LIMITED kupitia kinywaji chake cha Tusker, tumeweza kuona baadhi ya watanzania wakijitahidi kushiriki katika ushindani huo kwa hali na mali ili kuweza kufanikisha kuchukua ushindi huo lakini kwa bahati mbaya nchi yetu haijawahi kupata ushindi kutoka kwa hao wawakilishi wetu walioenda kushiriki katika TUSKER PROJECT FAME.

Kuna wawakilishi tofauti tofauti walioshiriki kuweza kuiwakilisha TZ mmoja wapo ni hemed, Alex, na wengine wengi.Lakini katika season hii ya nne tuliwakilishwa na Aneth pamoja na Leah Mou, Cynthia na Peter msechu na waliobahatika kufika nafasi nzuri katika shindano hili ni Leah,Aneth ambao walitoka hivi karibuni kwa kukosa kura za kutosheleza. Mpaka hivi sasa Tanzania bado inawakilishwa na Mwana kaka PETER MSECHU ambaye kwa wiki iliyopita aliingia katika probation  na kwa sasa anaelekea kutoka endapo waTanzania hatutashirikiana kumpigia kura ili aendelee kuwepo.
 Leah 
Aneth
Ni ombi langu kuwa ili muwakirishi wetu aendelee kubaki katika mashindano ni vyema tumpie kura ili azidi kuwepo na kufanya vizuri na mwisho wa siku arudi na ushindi nyumbani ili kufuta historia iliyopo katika mashindano hayo kwa TZ.
Jinsi ya kumpigia kura PETER MSECHU aendelee kuiwakilisha TANZANIA andika neno TUSKER 9 tuma kwenda 15522 kupitia kura yako utakuwa umeweza kumpa nafasi  PETER MSECHU kubaki katika TPF 4 na kuzidi kufanya vizuri na kurudi na ushindi.
WATANZANIA TUSHIRIKI KUPIGA KURA NA PIA TUOMBE MUNGU MUWAKIRISHI WA TANZANIA PETER MSECHU AFANYE VIZURI….