kwa mijibu wa chanzo chetu cha habari kinasema kuwa mkurugenzi wa mipango miji wa Missouri amechomoa ombi la waandaaji wa Concert hiyo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo makelele, Parking, na udhibiti wa watu watakao kuwepo siku hiyo. Mkurugenzi huyo pia amelalamika kuwa waandaaji wa Concert hiyo wanaendelea kupromote kuwa mtu mzima Nelly atapanda katika stage tarehe 21 August na pia tayari wameanza kuuza ticket za onyesho, huku wakitambua bado makubaliano hayajafikiwa.
Waandaaji wa Concert wamesema wanashangaa kuulizwa maombi mapya wakati tangu awali walishapeleka maombi, jamaa wanampango wa kukata rufaa kwa board ya jiji. Rufaa ya waandaji itaambatana na vielelezo vya mpangilio wa ulinzi utakavyo kuwa siku hiyo, pamoja na Documents zenye Signature za majirani wa eneo husika, wakithibitisha kuwa wao majirani wamebariki Concert hiyo kufanyika Branson.
inasemekana concert hiyo itaingizia mji wa Branson mapato ya dola za kimarekani laki tano.
hata sisi tunawashinda Branson, na huku ni Thousands of miles....
Kwa mujibu wa waandaaji wa Concert tayari mashabiki elfu tatu wamekwisha nunua Ticket ili Kumshuhudia Mtu mzima Nelly na kundi lake la Saint Lunatics wakishusha swager za Hip Hop kwa mara ya kwanza ndani ya mji wa Branson.

























